MENEJA wa klabu ya Schalke, Jens Keller amekiri kuwa anategemea vitu zaidi kutoka kwa Julian Draxler kufuatia kiungo huyo mshambuliaji kushuka kiwango katika kipindi cha karibuni. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa akipambana kufikia kiwango chake bora toka kuanza kwa mzunguko wa pili wa msimu na kuwa akisugua benchi tka kuanza kwa mwaka huu. Keller amemtaka chipukizi huyo kukazania kurejesha kiwango chake kama ilivyokuwa awali na kuachana na mambo mengine kwasasa. Keller amesema amefanya mazungumzo marefu na kinda huyo wiki hii na kumtaka kutobadilisha aina ya uchezaji wake aliokuwa nao mwanzoni kwani ndio umekuwa chanzo kikubwa cha kushuka kiwango chake. Draxler amecheza mechi 24 za Bundesliga msimu huu lakini amefunga bao moja pekee.
No comments:
Post a Comment