Friday, May 2, 2014

GIGGS AMUONDOA HOFU HODGSON KUHUSU ROONEY.

MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester United Wayne Rooney anatarajiwa kuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kinachonolewa na Roy Hodgson pamoja na kupata majeruhi hivi karibuni. Nyota huyo amepata majeruhi madogo ya kiuno na meneja wa muda wa United Ryan Giggs amesema anaweza kukosekana katika mchezo wa leo dhidi ya Sunderland. Majeruhi hayo yamekuja zikiwa zimebaki siku 10 kabla ya Hudgson hajateua kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Hata hivyo Giggs alimuondoa hofu Hodgson kwa kudai kuwa majeruhi yanayomkabili Rooney ni ya muda mfupi na atakuwa fiti kabla ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment