Friday, May 2, 2014

FARIA AFUNGIWA MECHI SITA.

MENEJA msaidizi wa klabu ya Chelsea, Rui Faria amefungiwa mechi sita kuhudhuria uwanjani kutokana na kuzozana na mwamuzi katika mchezo dhidi ya Sunderland ambao waliambulia kipigi cha mabao 2-1. Mreno huyo alimvamia mwamuzi Mike Dean baada ya Sunderland kuzawadiwa penati iliyowapa ushindi katika mchezo huo wa Ligi Kuu uliochezwa April 19 mwaka huu. Mara baada ya tukio hilo, Faria alitolea nje na baadae kukiri kufanya makosa mawili. Faria ambaye ana uwezo wa kukata rufani kupingana na adhabu hiya, mbali na kufungiwa lakini pia ametozwa faini ya paundi 30,000. Mara ya kwanza Faria kufanya kazi na Jose Mourinho ilikuwa wakati wote wakiwa wasaidizi wa Louis van Gaal katika klabu ya Barcelona mwaka 2000.

No comments:

Post a Comment