KLABU ya Manchester City imepiga hatua kubwa kuelekea kunyakuwa taji lao la pili la Ligi Kuu ndani ya miaka mitatu baada ya kuitandika Aston Villa na kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo. City wamekaa kileleni mwa msimamo kwa siku 11 pekee katika msimu mzima, lakini wanaongoza msimamo huo wakiwazidi mahasimu Liverpool kwa alama mbili na tofauto kubwa na mabao ya kufunga na kufungwa wakati timu zikitarajiwa kuchezwa mechi zake mwisho Jumapili. Sasa City watahitaji alama moja pekee wakati watakapoikaribisha West Ham United katika Uwanja wa Etihad, wakati Liverpool wao watakuwa wenyeji wa Newcastle United wakijua matumaini yao ya kunyakuwa ubingwa baada ya kupita miaka 24 hayatawezekana. Katika mchezo huo wa jana City iliigaragaza Villa kwa mabao 4-0 ambayo yote yalifungwa kipindi cha pili na Edin Dzeko aliyefunga mawili, Stevan Jovetic na Yaya Toure.
No comments:
Post a Comment