VYOMBO vya habari nchini Marekani vimemnukuu mmiliki wa timu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Clippers Donald Sterling akidai kuwa yeye sio mbaguzi na hatarajii kuiuza timu hiyo. Bilionea huyo alisikika katika mazungumzo yaliyorekodiwa na kuwekwa mtandaoni na RadarOnline akidai kuwa haamini kama wanweza kumlazimisha kuuza timu hiyo. Sterling alifungiwa maisha na Chama cha Mpira wa Kikapu nchini Marekani, NBA baada ya kurekodiwa akitoa kauli za kibaguzi. Jopo la Ushaurila NBA limekubaliana kuanza taratibu za kuiweka sokoni timu hiyo. Kamishna wa NBA, Adam Silver amesema Sterling mwenye umri wa miaka 81 atalazimika kuuza asilimia 75 ya hisa zake anazomiliki lakini anaweza kupinga kuuza mahakamani kwa mujibu wa mawakili wa michezo.
No comments:
Post a Comment