BEKI mahiri Rio Ferdinand amesisitiza kuwa hana mpango wa kustaafu hata kama atalazimishwa kuondoka Manchester United mwishoni mwa msimu huu. Mkataba wa sasa wa nahodha huyo wa zamani wa Uingereza unatarajiwa kuisha majira haya ya kiangazi na bado United hawajapanga kumpa mkataba mpya baada ya kushindwa kuwa katika mipango ya kocha aliyetimuliwa David Moyes. Mbali na kutokuwa katika mipango ya Moyes, beki huyo pia hakuwemo katika kikosi cha United kilichocheza mechi yake ya mwisho nyumbani dhidi ya Hull City wakiwa chini ya kocha wa muda Ryan Giggs ambaye inaaminika atampisha Loius van Gaal baada ya Kombe la Dunia. Pamoja na hayo Ferdinand ambaye alijiunga na United akitokea Leeds Julai mwaka 2002 kwa ada ya paundi milioni 30 anafikiri bado anaweza kuendelea kucheza pamoja na kutojua mustakabali wake Old Trafford.
No comments:
Post a Comment