MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa vilabu vilivyokiuka sheria ya kudhibiti matumizi ya fedha vinapaswa kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Klabu za Paris Saint-Germain-PSG na Manchester City zinakabiliwa na adhabu ya faini ya euro milioni 60 huku wakitakiwa kupunguza idadi ya wachezaji katika vikosi vyao vya Ligi ya Mabingwa kwa kukiuka sheria hiyo. Wenger anayefahamika kwa matumizi mazuri ya fedha anaona kunastahili adhabu zaidi kwa vilabu vinavyokiuka sheria hiyo. Kocha huyo amesema ili suala hilo lisiweze kurudiwa ni lazima adhabu kali za makusudi ziwekwe ikiwemo kuziondoa katika mashindano ya UEFA.
No comments:
Post a Comment