Monday, June 2, 2014

ARSENAL YAMFUNGIA VIOO FABREGAS.

KLABU ya Arsenal imeondoa uwezekano wa kumsajili Cesc Fabregas pamoja na mchezaji huyo kuwepo sokoni kwa ada ya paundi milioni 30. Fabregas ambaye alikuwepo jijini London kwa ajili ya kufanya tangazo la biashara mwishoni mwa wiki iliyopita anataka kurejea Uingereza na hivyo kuzivutia klabu za Liverpool na Chelsea. Barcelona wako tayari kumuuza kiungo huyo kwa paundi milioni 30 ambapo Arsenal ndio wenye nafasi ya kwanza ya kuweza kumsajili tena nahodha wake huyo wa zamani. Lakini inaaminika kuwa uwepo wa Mesut Ozil na Santi Cazorla katika kikosi cha Arsenal kumeifanya timu hiyo kuimarisha safu nyingine ikiwemo ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu ujao. Kwasasa klabu hiyo inapanga kuimarisha safu yake ya ulinzi kutokana na kiungo wake mkabaji Mikael Arteta akimalizia msimu wake wa mwisho, Arsenal wako tayari kumuwania Sven Bender wa Borussia Dortmund ili kuziba nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment