Monday, June 2, 2014

ROAD TO BRAZIL: ETO'O AMDHIHAKI MOURINHO TENA BAADA YA KUFUNGA BAO DHIDI YA UJERUMANI.

MSHAMBULIAJI nyota Samuel Eto’o kwa mara nyingine amemdhihaki Jose Mourinho baada ya kushangilia bao wakati timu yake ya taifa ya Cameroon ilipotoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ujerumani jana usiku. Mourinho alirekodiwa akizungumzia ubora wa washambuliaji wake katika sherehe ya wadhamini iliyofanyika nchini Switzerland Februari mwaka huu ambapo alidai kuwa Eto’o anaweza kuwa na umri mkubwa zaidi anaodai sasa. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33 alipofunga bao la kuongoza dhidi ya Ujerumani alirudia aina ya ushangiliaji aliyofanya katika mchezo kati ya Chelsea na Tottenham Hotspurs kwa kujifanya mzee. Pamoja na mahusiano mazuri waliokuwa nayo wawili hao wakati wakiwa Inter Milan, yaliyosaidia pia usajili wake kwenda Chelsea majira ya kiangazi mwaka jana, Et’o ameonekana kuchukizwa na kauli ya bosi wake huyo kwa kumfananisha na mpuuzi na kibaraka.

No comments:

Post a Comment