Thursday, June 19, 2014

ASHLEY COLE KUAMUA KWENDA BARCELONA AU AC MILAN.

BEKI wa zamani wa Uingereza, Ashley Cole anaangalia uwezekano wa kwenda katika klabu za Barcelona au AC Milan. Cole ambaye ameachwa na Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita amepewa ofa katika vilabu vyote viwili. Barcelona kwasasa wanahangaika kuziba nafasi ya beki wa kushoto ambapo mwishoni mwa msimu uliopita ilibidi wamtegemee sana nyota wa kimataifa wa Brazil Adriano. Lakini bado nafasi hiyo ilibakia kuwa na matatizo kufuatia kuuzwa kwa Eric Abidal kwenda Monaco katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi mwaka jana na Cole amekuwa chaguo la meneja mpya Luis Enrique. Milan pia pia wanatafuta wacheza wapya baada ya Filippo Inzaghi kuletwa kuchukua nafasi ya Clarence Seedorf kama kocha mpya wa timu hiyo. Cole aliamua kustaafu soka la kimataifa wakati kocha wa Uingereza Roy Hodgson alipoamua kumchukua beki wa Southampton Luke Shaw badala yake katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu.


No comments:

Post a Comment