Thursday, June 19, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: CHILE ITAISHANGAZA DUNIA - VIDAL.

KIUNGO wa timu ya taifa ya Chile, Arturo Vidal anaamini nchi yake inaweza kwenda mbali katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu na inaweza kuwa timu itakayowashangaza watu. Chile ambao wamepangwa kundi B walikuwa hawapewi nafasi ya kuingia hatua ya timu 16 bora katika michuano hiyo lakini ushindi wa mabao 3-1 waliopata kutoka kwa Australia katika mechi ya ufunguzi na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi Hispania umewahakikishia nafasi yao katika hatua inayofuata. Akihojiwa Vidal amesema timu yao ina damu changa yenye uchu wa ushindi hivyo anaamini wanaweza kwenda mbali na kuwashangaza wote katika michuano hiyo. Kwa upande wake amesema anajisikia vyema kutokana na kucheza vizuri dhidi ya Hispania na hilo lilikuwa jambo muhimu kwake. Chile itachuana na Uholanzi ambao nao wameshavuka hatua inayoafuata katika mchezo wa mwisho wa makundi utakaochezwa Jumatatu ijayo huko Sao Paulo.

No comments:

Post a Comment