Thursday, June 5, 2014

CHAMBERLAIN MAJANGA, AUMIA GOTI NA KUNA UWEZEKANO YAKAMKUTA YALIYOMKUTA WALCOTT.

KIUNGO wa kimataifa wa Uingereza, Alex Oxlade-Chamberlain anatarajiwa kufanyiwa vipimo katika goti lake leo kufuatia kuzuka hofu kuwa alipata majeraha katika msuli wa ndani ya goti. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 alitolewa nje kufuatia kukwatuliwa na Carlos Gruezo wakati wa mchezo wa kujipima nguvu kati ya Uingereza na Ecuador ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2. Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesema itakuwa pigo kubwa kama wakimpoteza kinda huyo kwenye michuano ya Kombe la Dunia iliyo mbele yao kwani ni mmoja kati ya wachezaji anaowategemea katika kikosi chake. Uingereza inatarajiwa kucheza mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Italia Juni 14 mwaka huu huko Manaus.

No comments:

Post a Comment