SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeendelea kuwa chini shinikizo kali kutoka kwa wadhamini wake wakuu kutokana na uamuzi wake kuipa uenyeji Qatar kuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Baada ya kampuni Sony kutangaza kutilia mashaka na kuomba uchunguzi zaidi juu ya tuhuma za ufisadi wakati wa uteuzi huo, kampuni za Adidas, Coca-Cola, Visa na Hyundai/Kia nazo zimeonyesha wasiwasi wake kuhusiana na suala hilo. Hatua inafanya kufikisha idadi ya kampuni tano kubwa kati ya sita zinazoidhamini FIFA kutoa taarifa kuhusiana na suala la Qatar huku kampuni moja pekee ya ndege ya Emirates wao wakikataa kutoa kauli yoyote. Kampuni ya mafuta ya BP na kampuni ya bia ya Budweiser ambao pia ni wadhamini wa Kombe la Dunia nao wametoa taarifa yao yakutaka ufafanuzi na uchunguzi zaidi katika jambo hilo. Qatar ilichaguliwa kuandaa michuano hiyo mwaka 2010 na kuzishinda nchi za Australi, Japan, Korea Kusini na Marekani katika kinyang’anyiro hicho.

No comments:
Post a Comment