MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani, LeBron James ameisaidia timu yake ya Miami Heat kwenda sawa na San Antonio Spurs kwa kila moja kushinda mechi moja ukiwa ni mchezo wa pili wa fainali ya Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini humo NBA. Katika mchezo huo wa pili James alifanikiwa kufunga vikapu 35 hivyo kuiwezesha timu yake ya Miami kushinda kwa vikapu 98 dhidi ya vikapu 96 vya Spurs. James mwenye umri wa miaka 29, alilazimika kutolewa nje wakati Miami walipokubali kipigo cha vikapu 110-95 kutoka kwa Spurs katika fainali ya kwanza. Mbali na James wachezaji wengine ambao waliisadia timu hiyo kwa kupata vikapu vingi zaidi ni Dwyane Wade na rashard Lewis ambao kila mmoja alifunga vikapu 14. Michuano hiyo ya NBA kwa kawaida huwa na mechi saba fainali na mshindi katika mechi nyingi zaidi kati ya hizo ndio huwatawadhwa bingwa.

No comments:
Post a Comment