VIONGOZI wa soka barani Ulaya wamemtaka rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter kutogombea kwa kipindi kingine kwasababu ya tuhuma za rushwa zinazoliandama shirikisho hilo. Ofisa Mkuu wa Chama cha Soka cha Uholanzi Michael Van Praag, amesema chini ya uongozi wa Blatter, FIFA imeandamwa na tuhuma za rushwa na ili ijisafishe ni sharti Blatter angatuke. Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Soka Uingereza , Greg Dyke,ameshtumu kauli ya Blatter kuwa madai ya rushwa kuhusiana na kuchaguliwa kwa Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia 2022 yanayoripotiwa katika magazeti ya Uingereza yamechochewa na ubaguzi wa rangi. Blatter anatarajiwa kutangaza nia yake ya kuwania nafasi kipindi cha tano kuingoza FIFA katika uchaguzi wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao. Kwa sasa wajumbe wa FIFA wana vikao huko Sao Paulo wakijiandaa kwa ufunguzi wa Kombe la Dunia hapo kesho ambako Sepp Blatter pia amekuwa akitoa cheche za maneno dhidi ya wale wanaoisema vibaya FIFA na Qatar.

No comments:
Post a Comment