Wednesday, June 11, 2014

MWAKA WA TABU KWA SCOLARI, AFIWA NA MPWAE.

MPWA wake kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari amefariki duniani jana kwa ajali ya gari ikiwa ni siku kabla ya michuano ya Kombe la Dunia. Kwa mujibu wa taarifa za polisi Tarcisio Joao Schneider mwenye umri wa miaka 48 alipata ajali hiyo karibu na mji wa Passo Fundo ambako ndiko nyumbani kwa Scolari. Huo ni msiba wa pili kwa kocha huyo katika wiki za hivi karibuni baada ya kuhudhuria msiba wa kaka yake wa kambo Mei mwaka huu. Scolari mwenye umri wa miaka 65 ambaye alishinda Kombe la Dunia akiwa na Brazil mwaka 2002, anatarajiwa kuingoza tena nchi hiyo katika michuano hiyo katika mchezo wa ufunguzi utakaochezwa jijini Sao Paulo kesho. Mbali na kuifundisha Brazil kwa vipindi viwili tofauti, Scolari pia amewahi kuifundisha Ureno, Chelsea, Bunyodkor na Palmeiras.

No comments:

Post a Comment