KOCHA wa timu ya taifa ya Algeria Vahid Halilhodzic amesisitiza kuwa Algeria hawajasahau utata uliopelekea kuenguliwa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1982 wakati wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Ujerumani katika hatua ya timu 16 bora. Sare ya bao 1-1 dhidi ya Urusi jana iliiwezesha Algeria kufuzu hatua hiyo kwa mara ya kwanza toka waanze kushiriki michuano hiyo. Ushindi wa Ujerumani Magharibi waliopata dhidi ya Austria miaka 32 iliyopita uliruhusu timu hizo kufuzu hatua inayofuata na kuiacha Alegria. Katika michuano hiyo ya mwaka 1982 Algeria walimaliza mechi zao tatu za makundi wakiwa wameshinda mara mbili na kufungwa moja lakini mabo yalibadilika katika mchezo wa mwisho kati ya West Germain na Austria ambapo mpaka leo inahisiwa suala la upangaji matokeo lilifanyika ili kuzifanya timu hizo kufuzu. Kocha Halilhodzic amesema hawajasahau tukio hilo kwasababu kila mtu amekuwa akizungumzia kuhusu Algeria na Ujerumani toka mwaka 1982. Maofisa wa soka wa Algeria walipinga na kudai mechi hiyo ilipangwa lakini tuhuma zao hazikuwahi kuthibitishwa, hata hivyo matokeo ya utata huo ndio yaliyopelekea mechi za mwisho za makundu katika michuano hiyo kuchezwa muda mmoja ili kuepusha suala la kupanga matokeo.
No comments:
Post a Comment