KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon, Volker Finke amesema anataka kutafuta chanzo kilichopelekea Benoit Assou-Ekotto kumpiga kichwa mchezaji mwenzake Benjamin Moukandjo wakati walipofungwa mabao 4-0 na Croatia. Wawili hao walikuwa wakizozana katika dakika za majeruhi kabla ya beki huyo wa Tottenham Hotspurs hajampiga kichwa mwenzake. Finke amesema aliona kilichotokea na anataka kujua ni nini haswa kilitokea mpaka wachezaji hao kugombana wenyewe kwa wenyewe. Wachezaji ilikuwa waendelee kugombana lakini Samuel Eto’o naye aliona tukio hilo na kuingilia kati kw akuwatenganisha wachezaji hao. Hilo limekuwa tukio la pili kwa Cameroon ambapo tukio la kwanza liliigharimu timu hiyo kucheza pungufu baada ya Alex Song kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga mgongoni mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic. Baadae Song aliomba radhi kwa tukio hilo ambalo liliiangusha timu yake pamoja na yeye mwenyewe na kuongeza kuwa lilikuwa jambo la kijinga ambalo halikupaswa kufanywa na mtu kama yeye.
No comments:
Post a Comment