Thursday, June 19, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: MASHABIKI WA MEXICO WACHUNGUZWA KWA UBAGUZI.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeanza kusikiliza kesi ya kinidhamu dhidi ya Mexico baada ya madai ya ubaguzi wa rangi uliofanywa na mashabiki wake wakati wa mchezo wa Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon Ijumaa iliyopita. Katika taarifa yake FIFA imesema imenzisha uchunguzi baada ya kile walichookiita tabia isiyo ya kiungwana ya mashabiki wa Mexico. Kutokana na sheria mpya zilizowekwa na FIFA mwaka jana ili kupambana na masuala ya ubaguzi wa rangi katika soka, kama Mexico wakikutwa na hatia mashabiki wake watalazimika kufungiwa kuingia uwanjani na kama wakiendelea kuna uwezekano wa kukatwa alama au hata kung’olewa katika michuano hiyo. Mbali na madai hayo FIFA pia inachunguza madai ya ubaguzi kutoka kwa mashabiki wa Brazil, Urusi na Croatia.

No comments:

Post a Comment