BEKI wa timu ya taifa ya Croatia, Dejan Lovren ameuponda uwezo wa mwamuzi Yuichi Nishirima baada ya kipigo walichopata katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Brazil jana na kudai kuwa timu yao ilikuwa ikicheza dhidi ya watu 12 huko Sao Paulo. Nishimura alitoa maamuzi yenye utata na yaliyozua maswali mengi kwa kutoa penati dhidi ya Lovren aliyetuhumiwa kumuangusha Fred, penati ambayo ilipigwa na Neymar na kuipa bao la pili Brazil. Neymar naye alikuwa na bahati na kukosa kupewa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko Luka Modric muda mfupi kabla nyota huyo wa klabu ya Barcelona haijafunga bao la kusawazisha, wakati bao la Croatia lilifungwa na Ivan Prisic likikataliwa kutokana na mwamuzi kudai golikpa Julio Cesar alifanyiwa faulo na Ivica Olic. Pamoja na matokeo kuwa mabao 3-1 baada ya Oscar kufunga bao lingine katika dakika za mwisho za mchezo, beki huyo wa Croatia anaonekana kutofurahishwa na maamuzi yaliyotolewa na Nishimura. Beki huyo anayecheza katika klabu ya Southampton amesema amesikitishwa mpaka anatamani kulia, kila ameona na ni kashfa kwa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Lovren amesema FIFA wamekuwa wakiwasisitiza suala la heshima huku wenyewe wakifanya tofauti, anadhani kombe hilo wangekabidhiwa wenyeji tu mara moja kama wataendelea kubebwa namna hiyo. Akiulizwa kama Croatia ingeweza kuifunga Brazil kama isingetolewa penati, Lovren aliongeza kuwa anadhani walicheza mchezo mzuri na walikuwa na uwezo wa kuifunga Brazil lakini sio dhidi ya watu 12.
No comments:
Post a Comment