KLABU ya Barcelona imedai kuwa kiwango cha Cesc Fabregas kilikuwa kinaporomoka wakati akiitumikia timu hiyo baada ya nyota huyo kusajiliwa na Chelsea. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 alikulia katika shule ya Barcelona ya La Masia kabla ya kwenda Arsenal na baadae kurudi tena katika klabu ayke ya utotoni kwa ada ya paundi milioni 34 Agosti mwaka 2011. Hata hivyo katika taarifa ya klabu hiyo waliyotoa katika mtandao wao wamedai kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa akishindwa akishindwa kucheza kwa kiwango cha juu katika msimu wa pili wa ligi. Taarifa ya klabu hiyo iliendelea kudai kuwa pamoja na kuelewa vyema mfumo wa timu hiyo lakini kila msimu amekuwa akishuka kiwango chake ndio maana wameamua kumuachia. Fabregas amefunga mabao 42 katika mechi 151 alizoichezea Barcelona katika kipindi cha miaka mitatu na kuisaidia timu hiyo kunyakuwa taji la La Liga na Kombe la Mfalme.
No comments:
Post a Comment