Friday, June 13, 2014

SAGNA ATANGAZA KUIKACHA ARSENAL.

BEKI wa klabu ya Arsenal, Bacary Sagna akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil, ametangaza kuwa miaka saba aliyoitumikia klabu hiyo imetosha. Kwa mujibu wa vyombo vya habari, beki huyo mwenye umri wa miaka 31 yuko mbioni kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu klabu ya Manchester City. Sagna aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wake wa kijamii wa twitter akidai kuwa hajui aanzie wapi kusema lakini anataka kuwashukuru sana Arsenal kwani imekuwa ni kama familia yake na amejifunza mengi katika kipindi cha miaka saba. Sagna aliendelea kudai kuwa kwasasa ni muda wake wa kuondoka na kwa mara nyingine anawashukuru sana. Mchezaji huyo alijiunga na Arsenal akitokea Auxerre mwaka 2007 na alifanikiwa kushinda taji lake la kwanza akiwa Emirates wakati Arsenal ilipoitandika Hull City katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA uliofanyika Wembley mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment