MENEJA wa klabu ya Everton, Roberto Martinez amesaini mkataba mpya wa miaka mitano ambao utamfanya kuendelea kuinoa timu hiyo yenye maskani yake Soodison Park mpaka 2019. Kocha huyo raia wa Hispania alitua Merseyside majira ya kiangazi mwaka jana na amekuwa na msimu mzuri katika Ligi Kuu kwa kuiwezesha timu hiyo kushika nafasi za juu katika msimamo wa ligi huku akikosa kidogo nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Martinez ambaye pia amewahi kuinoa Wigan Athletic anataka kuiboresha zaidi timu hiyo msimu ujao baada ya kusaini mkataba wa muda mrefu. Akihojiwa Martinez amesema maefurahishwa kwa kupata nafasi hiyo na kuahidi kuisuka zaidi timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao ili waweze kufanya vyema zaidi ya msimu uliopita. Mwenyekiti wa Everton Bill Kenwright naye alifurahishwa na kusainiwa kwa mkataba huo na kudai kuwa Martinez ni mmoja kati ya makocha bora duniani kwasasa na kila timu inamuhitaji.

No comments:
Post a Comment