Wednesday, June 18, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: KOCHA WA ALGERIA AFADHAISHWA KWA KUKOSA USHINDI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Algeria, Vahid Halilhodzic ameeleza kusikitishwa kwake na kupoteza mchezo dhidi ya Ubelgiji kwa kufungwa mabao 2-1, mchezo ambao ulikuwa wa ugunguzi kwa kundi H jana. Algeria ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Sofiane Feghouli lakini aina yao ya mchezo wa kuzuia ilishindwa kufanya kazi na kujikuta wakifungwa. Kocha huyo amesema amesikitishwa kwa kushindwa kuchukua ushindi huo muhimu ambao ungekuwa na msaada mkubwa kwa timu yao. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kipindi cha pili waliwaruhusu sana Ubelgiji kuingia katika eneo lao la hatari jambo ambalo limewagharimu na kujikuta wakipoteza mchezo. Algeria inatarajiw akukwaana na Korea Kusini katika mchezo wao ujao utakaochezwa Jumapili huko Porto Alegre.

No comments:

Post a Comment