AL AHLY BADO YASAKA KOCHA.

KLABU kongwe ya Misri Al Ahly bado wanatafuta kocha mpya wa kuingoza timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao baada ya kumtimua kocha wao wa zamani Mohamed Yousef. Klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la Cairo limetaja majina matatu ya makocha watakaogombania nafasi hiyo huku wakitaraji kutaja jina la kocha wiki ijayo kuchukua nafasi ya kocha wa muda Fathy Mabrouk. Mabingwa hao watetezi wa michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika, wamefikia mahali pazuri katika mzungumzo na kocha Paulo Duarte wa Ureno huku vyanzo vya karibu na timu hiyo vikidai kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 tayari amekubali kibarua hicho lakini bado hawajafikia muafaka kwenye mambo ya fedha. Chanzo hichohicho kimedai kuwa Al Ahly wamempa ofa ya dola 30,000 kwa mwezi lakini kocha huyo anaonekana kutaka zaidi. Al Ahly pia wanawapa nafasi kocha Milovan Rajevac wa Serbia ambaye aliifundisha Ghana katika michuano ya Kombe la Dunia 2010 pamoja na mchezaji wao wa zamani Mokhar Mokhar ambaye kwasasa anafundisha timu ya Petrojet.
No comments:
Post a Comment