Wednesday, June 18, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: MABAO MATANO BORA YALIYOFUNGWA KATIKA MICHUANO HIYO MPAKA HIVI SASA.

MECHI za ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Brazil zimetengeneza mabao kadhaa mazuri na yafuatayo ni mabao tano bora ambayo yaliwaacha mashabiki midomo wazi. Bao la kwanza ni la Robin van Persie aliyefunga katika ushindi wa timu yake ya Uholanzi wa mabao 5-1 dhidi ya Hispania. Katika mchezo huo Hispania ndio waliotangulia kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Xabi Alonso aliyefunga kwa panati lakini bao la kusawazisha la Van Pesrie aliyepiga kichwa mbali na kumuacha kipa Iker Casillas lakini pia liliwaacha mashabiki wengi midomo wazi kwa ubora wake. Akihojiwa kuhusiana na bao hilo Van Persie mwenye amesema lilikuwa bao zuri lakini anakiri alifanya kama anacheza kamari baada ya kumuona Casillas ametoka langoni ila anashukuru uamuzi wake ulikuwa na mafanikio. Bao lingine ni lile lililofungwa na mshambuliaji nyota wa Argentina Lionel Messi katika ushindi waliopata wa mabao mawili 2-1 dhidi ya Bosnia, bao ambalo limemaliza ukame wa mabao kwa nyota huyo uliodumu kwa miaka nane. Mara ya mwisho Messi kufunga bao katika michuano ya Kombe la Dunia ilikuwa ni katika mchezo dhidi ya Serbia & Montenegro kabla hazijatengana miaka nane iliyopita ambapo Argentina ilishinda kwa mabao 6-0. Bao lingine ni la Haris Seferovic wa Switzerland ambalo liliiwezesha timu yake hiyo kuifunga Ecuador mabao 2-1 likifuatiwa na la nahodha wa Marekani Clint Dempsey alilofunga katika mchezo dhidi ya Ghana na kuweka rekodi ya kuwa bao la mapema zaidi katika michuano hiyo. Bao la mwisho lililowaacha mashabiki midomo wazi ni la Arjen Robben wa Uholanzi katika mechi hiyo ambapo vyombo vya habari vimeripoti kuwa mshambuliaji huyo alikuwa akikimbia kwa mwendo wa kilometa 37 kwa sasa wakati akienda kufunga ukiwa ni mwendo wa haraka zaidi kurekodiwa na FIFA katika mechi zake. Mwanaridha Usain Bolt pekee ndiye angeweza kumzuia Robben kama angekuwa mchezaji maana ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa na kasi zaidi kwa kukimbia mwendo wa kilometa 45 kwa sasa wakati akiweka rekodi ya dunia katika mashindano la riadha yaliyofanyika Berlin mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment