Wednesday, June 18, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: PIGO URENO KWA KUMKOSA COENTRAO.

BEKI mahiri wa timu ya taifa ya Ureno, Fabio Coentrao anatarajiwa kukosa mechi zote zilizosalia za michuano ya Kombe la Dunia kutokana na kupata mejeruhi ya msuli. Beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 26 anayecheza katika klabu ya Real Madrid alitolewa nje katika kipindi cha pili kwenye mchezo wa kundi G ambao walifungwa na Ujerumani mabao 4-0. Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Ureno imedai kuwa baada ya mchezaji huyo kufanyiwa vipimo jana imegundulika kuwa hataweza kuwa fiti kwa wakati ili aweze kuendelea na michuano hiyo. Mshambuliaji Hugo Almeida na golikipa Rui Patricio ambao wote nao walikuwa majeruhi pia walifanyiwa vipimo jana lakini hakuna yoyote aliyeondolewa katika michuano hiyo. Kipigo kizito walichopata Ureno kumewaacha mkiani mwa kundi G kuelekea katika mechi zake dhidi ya Marekani na Ghana.

No comments:

Post a Comment