MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Uingereza, Raheem Sterling amesisitiza kuwa anafurahi kubadilishana nafasi na Wayne Rooney kama itaisaidia timu yao kuweka matumaini ya kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Dunia. Sterling mwenye umri wa miaka 19, alichezeshwa nyuma ya Daniel Sturridge katika kipigo cha mabao 2-1 walichopata kutoka kwa Italia na alipata pongezi kwa kiwango bora alichoonyesha katika mchezo huo. Rooney yeye alichezeshwa wingi ya kushoto lakini pamoja na kutengeneza bao la kusawazisha watu wengi hawakufurahishwa na kiwango chake hivyo kocha Roy Hodgson amepanga kumrejesa katika nafasi ya mshambuliaji wa kati aliyozoea. Akihojiwa kuhusiana na hilo Sterling amesema atafurahi kupangwa nafasi yoyote kocha atakayoona inamfaa. Wachambuzi wa soka wa BBC ambao pia waliwahi kuwa wachezaji na manahodha wa Uingereza, Alan Shearer na Rio Ferdinand wamemtaka Hodgson kumchezesha Rooney katikati kwenye mchezo huo muhimu ambao kama wakishindwa safari ya mapema itakuwa imewadia.
No comments:
Post a Comment