Monday, June 2, 2014

ONAZI AKANUSHA KASHFA YA UPANGAJI MATOKEO.

MCHEZAJI wa kimataifa wa Nigeria, Ogenyi Onazi amekanusha kuhusika na sakata la upangaji matokeo ya mechi baada ya kutajwa kuhusika katika njama hizo. Onazi mwenye umri wa miaka 21 alipigwa picha za video zilizotolewa na gezeti la The Sun la nchini Uingereza akikutana na wakala wake Henry Chukwuma Okoroji na watu wanaotuhumiwa kuwa wapangaji wa matokeo. Onazi anayecheza katika klabu ya Lazio ya Italia aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter jana usiku akisisitiza kuwa alikatana na wakala wake huyo kwa ajili ya kuzungumzia masuala yake yanayomhusu. Kiungo huyo aliendelea kudai kuwa hana mahusiano yoyote na watu au kikundi kinachojishughulisha na masuala hayo ya upangaji matokeo.

No comments:

Post a Comment