MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Colombia, Radamel Falcao anatarajiwa kuikosa michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuachwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 wa nchi hiyo. Mchezaji mwenye umri wa miaka 28 anayekipiga katika klabu ya Monaco hajacheza mechi yoyote toka alipoumia msuli wa goti Januari mwaka huu. Kocha wa Colombia, Jose Pekerman alimjumuisha nyota huyo katika kikosi chake cha wachezaji 30 wa awali kwa matumaini kwamba anaweza kupona kwa wakati. Lakini Falcao ambaye alifunga mabao tisa yaliyoiwezesha nchi hiyo kufuzu michuano hiyo ameonekana kushindwa kupona kwa wakati hivyo kocha kuamua kumuacha. Colombia imepangwa katika kundi C sambamba na timu za Ugiriki, Ivory Coast na Japan.
Kikosi kamili ni
Makipa: David Ospina (Nice), Faryd Mondragon (Deportivo Cali), Camilo Vargas (Independiente Santa Fe).
Mabeki: Mario Yepes (AC Milan), Cristian Zapata (AC Milan), Pablo Armero (West Ham, on loan from Napoli), Camilo Zuniga (Napoli), Santiago Arias (PSV Eindhoven), Eder Alvarez Balanta (River Plate), Carlos Valdes (San Lorenzo).
Viungo: Fredy Guarin (Inter Milan), Juan Cuadrado (Fiorentina), James Rodriguez (Monaco), Abel Aguilar (Toulouse), Juan Fernando Quintero (Porto), Carlos Sanchez (Elche), Aldo Leao Ramirez (Morelia), Alexander Mejia (Atletico Nacional).
Washambuliaji: Victor Ibarbo (Cagliari), Jackson Martinez (Porto), Carlos Bacca (Sevilla), Adrian Ramos (Hertha Berlin), Teofilo Gutierrez (River Plate).

No comments:
Post a Comment