HATMA ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 inatarajiwa kuamuliwa ndani ya wiki kadhaa baada ya mtu anayeongoza uchunguzi wa ndani kujua ni jinsi gani Qatar walishinda haki ya kuandaa michuano hiyo atakapotoa taarifa ya uchunguzi wake Julai mwaka huu. Mwanasheria wa zamani wa Marekani, Michael Garcia ndio anaonekana kushikilia mstakabali wa Qatar waliotenga mabilioni ya dola kwa ajili ya michuano hiyo baada ya tuhuma mpya za ufisadi hivyo kuamuliwa michuano hiyo ihamishwe kama masuala hayo ya ufisadi yatathibitishwa. Katika taarifa yake Garcia amesema amepanga kutoa ripoti kamili kuhusiana na tuhuma hizo baada ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil kumalizika. Garcia ambaye ni kiongozi wa kamati ya uchunguzi ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwasasa yuko Mashariki ya Kati na anategemewa kukutana na maofisa wa soka wa Qatar ili kuhusiana na sakata hilo.
No comments:
Post a Comment