MENEJA mpya wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal amekiri kuwa alikaribia kuchukua mikoba ya kuinoa klabu ya Tottenham Hotspurs kabla ya ya nafasi hiyo kutolewa Old Trafford. Wakati kibarua cha Tim Sherwood kikwia mashakani wakati wa mzunguko wa pili wa msimu wa 2013-2014, kocha huyo wa timu ya taifa ya Uholanzi alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kutua White Hart Lane. Lakini baada ya David Moyes kutimuliwa na United, Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 62 alipewa ofa ya kibarua hicho na kumuacha kocha wa Southamton Mauricio Pochettino akichukua kibarua cha kuinoa Spurs mwishoni mwa msimu. Van Gaal amesema wakati akiwa mdogo alikuwa mshabiki mkubwa wa Spurs enzi hizo ikiwa chini ya Jimmy Greaves. Kuchoa huyo aliendelea kudai kuwa kutokana na mapenzi hayo aliyokuwa nayo ilibaki kidogo akubali kuinoa timu hiyo yenye maskani yake kaskazini mwa jiji la London.
No comments:
Post a Comment