Tuesday, June 3, 2014

UEFA YAMUWEKEA KIGINGI BLATTER.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limeweka wazi kwa mataifa wanachama kuwa hawataunga mkono nia ya Sepp Blatter kuogombea urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kipindi cha tano. Inaaminika kuwa UEFA hawataki kuwa sehemu ya msimamo wowote wa Blatter katika mkutano wa mwaka wa FIFA kama atatangaza kutetea kiti chake hicho katika uchaguzi ujao. Blatter mwenye umri wa miaka 78 raia wa Switzerland amekuwa akishikilia nafasi hiyo toka alipochaguliwa mwaka 1998. Katika kipindi cha karibuni Blatter amedokeza kuwa anaweza kuamua kutetea kiti chake katika uchaguzi utakaofanyika mwakani. Kama akiamua kugombea kipindi kingine itakuwa kama anavunja ahadi yake aliyoitoa katika mkutano mkuu wa UEFA mwaka 2011 ambapo alidai kipindi hiki kitakuwa cha mwisho kwake kuliongoza shirikisho hilo.

No comments:

Post a Comment