Monday, June 2, 2014

ROAD TO BRAZIL: MAJERAHA YANAMUUMIZA ROBERY - GIROUD.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ufaransa, Olivier Giroud amedai kuwa mchezaji mwenzake Franck Ribery ana hasira na woga juu ya nafasi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia. Giroud alicheza kwa dakika zote tisini katika mchezo wa kirafiki karafiki kati ya Ufaransa na Paraguay ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 huko jijini Nice lakini Ribery anayecheza Bayern Munich hakujumuishwa katika kikosi hicho kutokana na kuendelea kujiuguza majeraha ya mgongo. Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, Noel Le Graet alifafanua wiki iliyopita kuwa Ribery hayuko katika nafasi ya kuikosa michuano hiyo kufuatia vipimo alivyofanyiwa lakini Giroud amesema nyota mwenzake huyo tayari ameingiwa na woga kufuatia mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Honduras Juni 15 kukaribia. Giroud amesema tayari Ribery ameanza kugadhabishwa na kuingiwa na woga kuhusiana na suala hilo hivyo wakiwa kama watu wake wa karibu kwasasa ni kumsadia kwa kumtuliza na kumuomba avute subira.

No comments:

Post a Comment