Monday, June 2, 2014

ROAD TO BRAZIL: SCOLARI AKASIRISHWA NA MAANDALIZI YA KIKOSI CHAKE.

KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scolari amekiri mazoezi ya jana hayakwenda sahihi na kudai bado mpaka sasa hajapanga kikosi cha kwanza kwa timu hiyo. Scolari aligawanya kikosi cha wachezaji wake 23 katika timu mbili mara kadhaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajili ya mechi za kujipima nguvu huku kocha huyo mwenye umri akitumia nafasi hiyo kujaribu wachezaji tofauti kwa ajili ya kutafuta kikosi cha kwanza. Lakini baada ya mazoezi ya jana huko Teresopolis, Scolari ameeleza kuwa anaweza kufikiria tena kuhusu kikosi cha kwanza kuelekea michuano ya Kombe la Dunia baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Panama utakaochezwa kesho. Scolari amesema hajafurahishwa na mazoezi ya timu hiyo mpaka sasa na kama hujapenda kitu anatakiwa kutafuta majawabu mpaka atakaporidhika kwamba kikosi hicho kinafanya vile anavyoona ni sawa.

No comments:

Post a Comment