Thursday, June 19, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: RONALDO BADO MAJANGA.

VYOMBO vya habari nchini Ureno vimeripoti kuwa Cristiano Ronaldo aliondoka mapema mazoezini na kuwaacha wachezaji wenzake wa timu ya taifa wakiendelea na aliondoka uwanjani akiwa amefungwa barafu katika goti lake. Picha zilizotumwa katika mtandao wa michezo wa Record zimemuonyesha Ronaldo akitembea huku akiwa na bandeji kubwa lililofungwa na barafu katika goti lake la kushoto na kulikuwa hakuna kauli yoyote kutoka kwa Shirikisho la Soka la Ureno. Ronaldo amekuwa akisumbuliwa na majeruhi wakati wa wiki za mwisho za msimu uliopita akiwa na timu yake ya Real Madrid kabla ya kucheza kwa dakika 120 katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid. Baada ya hapo nyota huyo alipumzishwa wakati wa mazoezi ya awali ya maandalizi ya Kombe la Dunia baada ya kuonekana kuwa na mejeraha ya msuli na baadae goti la kushoto. Kutokana na hilo kumekuwa na mashaka makubwa kwa nyota huyo kucheza katika mchezo dhidi ya Marekani utakaochezwa Jumapili hii.

No comments:

Post a Comment