Friday, June 13, 2014

RONALDO WATOA HOFU MASHABIKI WA URENO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo ameviambia vyombo vya habari nchini kwake jana kuwa majeraha ya goti lake la kushoto yamepona, wakati akifanya mazoezi. Zaidi mashabiki wapatao 10,000 walikuwepo kutizama mazoezi hayo ya wazi huko Campinas ambapo kuna wakati mwanamke mmoja alikimbia uwanjani na kujaribu kumfikia Ronaldo na kuzuiwa na walinzi kabla ya kukimbia tena mita 40 na kuwekwa chini na walinzi wengine. Ronaldo ambaye alicheza mchezo wa kirafiki ambao Ureno iliitandika Ireland kwa mabao 5-1, alimfuata mwanamke huyo aliwekwa chini ya ulinzi na kuweka saini katika fufala yake kabla ya wachezaji wengine wa Ureno nao kuvua fulana zao na kuwarushia mashabiki hao. Ureno itakwaana na Ujerumani katika mchezo wao ufunguzi utakaochezwa Jumatatu.

No comments:

Post a Comment