WADHAMINI wakubwa wa timu ya taifa ya Nigeria, wameamua kusimamisha udhamini wao kutokana na kusimamishwa kwa Aminu Maigari na bodi ya Shirikisho la Soka la nchi hiyo-NFF. Kampuni kubwa ya vifaa vya michezo ya Adidas imeamua kukatiza udhamini wake mara moja na kueleza kusikitishwa kwao na mgogoro unalitafuna shirikisho hilo kwasasa. Uamuzi huo wa Adidas ambao wamekuwa wakitengeneza jezi za timu hiyo kwa zaidi ya miaka kumi sasa unakuja ikiwa ni siku chache zimepita toka Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kuwapa onyo la kuwafungia kutokana na serikali ya nchi hiyokuingilia masuala ya soka. Wiki iliyopita mahakama ya mji wa Jos nchini humo iliitaka kamati nzima ya utendaji ya NFF kujiuzulu wakati waziri wa michezo akimteua Lawrence Katken kuchukua uongozi wa muda mpaka utakapoitishwa uchaguzi mpya. Siku chache baadae kulifanyika mkutano mkuu wa dharura jijini Abuja na kuiengua kamati hiyo ya utendaji hatua ambayo imepingwa vikali na FIFA.
No comments:
Post a Comment