Monday, July 7, 2014

KOCHA WA ALGERIA AJIUZULU PAMOJA NA KUPOKEWA KISHUJAA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Algeria, Vahid Halilhodzic amethibitisha kujiuzulu rasmi kibarua chake pamoja na kuombwa kuendelea kubakia baada ya kulivusha taifa hilo katika hatua ya mtoano ya michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza. Kocha huyo raia wa Bosnia alithibitisha kuoondoka katika taarifa iliyotolewa katika mtandao wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo. Halilhodzic alipata maombi binafsi kutoka kwa rais wan chi hiyo Abdelaziz Bouteflika kuendelea kuinoa timu hiyo baada ya kikosi kuwasili na kukaribishwa kishujaa jijini Algiers Jumatano iliyopita. Algeria alichapwa mabao 2-1 na Ujerumani katika muda wa nyongeza kwenye hatua hiyo ya mtoano mchezo ambao ulichezwa huko Porto Alegre Jumatatu iliyopita. Katika taarifa yake, kocha huyo amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupata ushauri kutoka kwa familia yake na pia kutaka changamoto mpya.

No comments:

Post a Comment