Monday, July 7, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: DI MARIA KUIKOSA UHOLANZI.

DAKTARI wa timu ya taifa ya Argentina amebainisha kuwa winga Angel Di Maria ataukosa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Uholanzi Jumatano lakini kuna uwezekano mshambuliaji Sergio Aguero akarejea tena uwanjani baada ya kupona majeruhi. Di Maria mwenye umri wa miaka 26 alicheza dakika 33 pekee katika mchezo war obo fainali dhidi ya Ubelgiji mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo walishinda kwa bao 1-0. Daktari Daniel Martinez amesema mara baada ya mchezaji huyo kufanyiwa vipimo jana kuwa kuna uwezekano akapona kwa wakati kabla ya mchezo wa fainali lakini akakiri kuwa hakuna nafasi ya Di Maria kucheza katika mechi dhidi ya Uholanzi. Lakini wakati kukiwa na habari mbaya kuhusu Di Maria kocha Alejandro Sabella anaweza kuwa na ahueni kutokana na taarifa za Aguero kupona majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua.

No comments:

Post a Comment