BLATTER ADAI MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA NCHINI BRAZIL ILIFANIKIWA ZAIDI KULIKO AFRIKA KUSINI.
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ameipa michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu iliyoandaliwa nchini Brazil alama 9.25 kati ya alama 10. Blatter amesema Brazil imeizidi Afrika Kusini ambayo aliipa alama 9 baada ya kuandaa michuano hiyo mwaka 2010. Kulikua na hofu kubwa kuhusu suala la usalama, usafiri na viwanja lakini mambo yote hayo hayakutokea kama yalivyohofiwa na badala yake maajabu yalipatikana ndani ya viwanja. Moja ya maajabu hayo ni mabingwa watetezi kulambwa mabao 5-1 na Uholanzi huku timu zilizokuwa hazipewi nafasi za Costa Rica, Algeria na Colombia zote ziking’ara katika hatua makundi. Hayo na mengine mengi yaliyotokea ndio yanamfanya Blatter kuamini kuwa Brazil imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika michuano hiyo inayochezwa mara moja kila baada ya miaka minne. Blatter amesema ni mategemeo yake wenyeji wa michuano inayofuata mwaka 2018 nchini Urusi na ile ya mwaka 2022 nchini Qatar watakuwa wamepata uzoefu wa kutosha kutokana na michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment