BINGWA wa zamani wa dunia wa mbio za mita 100, Asafa Powell na Mjamaica mwenzake Sherone Simpson wamepunguziwa vifungo vyao kutoka miezi 18 mpaka miezi sita. Kutokana na uamuzi huo uliotolewa na Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa ya Michezo-CAS, inamaanisha kuwa wawili wanaweza kurejea uwanjani mapema iwezekanavyo. Powel amepanga kukimbia katika mashindano ya Diamond League yatakayofanyika huko Lucerne baadae leo. Powell na Simpson ambao walishinda medali za dhahabu katika mbio za kupokezana vijiti kwenye olimpiki, wote walikutwa na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli mwaka jana katika michuano ya taifa ya Jamaica. Wote wawili walikana kutenda kosa hilo kwa kudhamiria hivyo kukata rufani CAS ili waweze angalau kupunguziwa adhabu kubwa wlaiyopewa.

No comments:
Post a Comment