KOCHA wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah ameapa kutomuita tena Kevin-Prince Boateng katika kikosi chake baada ya kupishana kauli katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil. Wakiwa wamerejea nyumbani baada ya kutolewa katika michuano hiyo, Appiah amesema kwasasa atachagua wachezaji ambao wana nidhamu, wanajitoa na waliopo tayari kufia nchi yao. Na kwa kuongezea hilo Appiah amesema Boateng hawezi kuwa sehemu ya mipango yake hiyo kwasababu anaamini katika nidhamu kwa wachezaji ili timu iweze kufanya vyema. Boateng alitimuliwa katika kikosi cha Black Stars wakati kikiwa katika maandalizi ya mchezo wake wa mwisho wa makundi dhidi ya Ureno baada ya kumtukana Appiah wakati wakiwa mazoezini. Mbali na Boateng kiungo Sulley Muntari naye alitimuliwa kambini baada ya kumpiga ofisa wa soka wa Ghana baada ya kupishana kauli.
No comments:
Post a Comment