Thursday, July 3, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: NEYMAR AWABEEP SONY KWA KUTINGA HEADSPHONE ZA BEATS BY DRE KATIKA MKUTANO NA WAADHISHI WA HABARI.

MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar amezua jambo katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini humo kwa kuonekana akiwa amevaa spika za masikioni aina ya Beats ambazo zimekatazwa kutumiwa na wachezaji katika michuano hiyo. Nyota huyo alionekana amezivaa spika hizo katika mkutano na waandishi wa habari jana kuelekea katika mchezo wao wa robo fainali dhidi ya Colombia utakaochezwa kesho. Tukio limekuja baada ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kukubaliana na kampuni ya Sony kuwa na haki katika kipindi chote cha mwezi mzima wa michuano hiyo. Neymar alikuwa akizungumza katika kambi ya timu yao iliyopo Teresopolis kabla ya mchezo huo ambapo mpaka sasa FIFA wenyewe hawazungumzia tukio hilo. Wachezaji wote kutoka mataifa 32 yanayoshiriki michuano hiyo walipigwa marufuku kutumia bidhaa zinzotengenezwa na Beats wakati wakizungumza na vyombo vya habari na siku ya mechi ambapo wote walipewa spika kutoka kampuni ya Sony bure lakini ni wachache walioonekana kuzitumia.

No comments:

Post a Comment