KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester City, Samir Nasri amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na timu hiyo. Nasri mwenye umri wa miaka 27 alikuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa ambao alisaini alipojiunga na klabu hiyo akitokea Arsenal mwaka 2011. Makubaliano yalikuwa tayari yameshafikiwa kabla ya Nasri ambaye hakuchaguliwa katika kikosi cha Ufaransa kilichoshiriki michuano ya Kombe la Dunia, hajaondoka kwenda katika mapumziko ya majira ya kiangazi. Nasri aliuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa amefurahishwa na kusaini mkataba huo mpya mrefu ambao utamfanya kuendelea kuwepo City mpaka mwaka 2019.

No comments:
Post a Comment