Thursday, July 10, 2014

MOURINHO AMPONDA KLOSE, ADAI HAWEZI KUFIKIA UBORA WA RONALDO.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amempongeza Miroslav Klose kwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika michuano ya Kombe la Dunia lakini amedai kuwa haweza kumfikia nguli wa Brazil Ronaldo kwa ubora. Klose mwenye umri wa miaka 36 alifunga bao wakati Ujerumani ikiididimiza Brazil kwa mabao 7-1 hivyo kuongeza idadi yake ya mabao kufikia 16 katika michuano hiyo akimzidi bao moja Ronaldo. Mabao yote hayo aliyofunga Klose katika michuano hiyo amefunga akiwa ndani la eneo la penati tofauti na Ronaldo ambayo mabao yake amefunga kwa mashuti ya mbali, juhudi binafsi na mengine aliyofunga kwa karibu wakati wa kipindi chake akicheza soka. Kutokana na matokeo hayo, Mourinho amesikitishwa kuona nyota huyo wa zamani wa Barcelona na Real Madrid akipoteza rekodi yake ya mashindano hayo na kubainisha kuwa kuna mchezaji mmoja pekee ndiye anayedhani anaweza kumpita Ronaldo kwa viwango katika historia ya mchezo huo. Mourinho amesema anaheshimu kwa mafanikio hayo aliyopata Klose lakini bado Ronaldo anabakia kuwa mmoja wa wachezaji anawaheshimu baada ya Diego Maradona.

No comments:

Post a Comment