Friday, July 18, 2014

DA SILVA WA ZAMALEK AFUNGIWA MECHI TATU NA CAF.

KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF, limefungia mechi tatu mchezaji wa Zamalek, Dominique Da Silva na kumtoza faini ya dola 5,000. Wachezaji Hazem Emam na Mahmoud Abdel Rahem wao wamefungiwa mechi moja kimammoja kufuatia tukio lililotokea katika mchezo wa mondo wa tatu wa hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe uliochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Lubumbashi. Wachezaji hao walikimbia uwanjani mwishoni mwa mchezo na kumshambuliaji mwamuzi Josph Lambty kutoka Ghana kutokana na kutoridhishwa na baadhi maamuzi. Kumekuwa na taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo kuwa benchi la ufundi linaweza kumptimua Da Silva baada ya adhabu hiyo iliyotolewa na CAF itakayomfanya kutocheza mpaka mwisho wa hatua ya makundi ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment