KOCHA mpya wa klabu ya Juventus, Massimiliano Allegri amesisitiza kuwa hana tatizo na kiungo Andrea Pirlo kufuatia uteuzi wake huo. Pirlo na Allegri wamekuwa katika msuguano toka kiungo huyo alipoondoka Ac Milan katika usajiliwa majira ya kiangazi mwaka 2011, ambapo nyota huyo wa kimataifa wa Italia alimtuhumu kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 kuwapa nafasi Massimo Ambrosini na Mark van Bommel hatua ambayo ilimlazimu kuondoka. Kiungo huyo mahiri alijiunga na Juventus na kuisaidia kunyakuwa mataji matatu mfululizo ya Serie A lakini uteuzi wa Allegri aliyechukua nafasi ya Antonio Conte unamaanisha wawili hao watakutana tena baada ya kuachana kwa miaka mitatu. Akihojiwa Allegri amesema amkuwa na mahusiano mazuri na Pirlo toka wakati akiwa Milan na kuongeza kuwa mara nyingi alikuwa akisumbuliwa majeruhi akiwa huko lakini wakati akiwa fiti alikuwa akimpa nafasi ya kucheza. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa zaidi ya hilo hakuwahi kuwa na tatizo naye kwani kama angehoji kuhusu ubora wake kila mtu angemuona mpuuzi kutokana na kiwango kikubwa alichokuwa nacho. Mkataba wa Pirlo na Juventus unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.
No comments:
Post a Comment