DEREVA mahiri wa mashindano langalanga kutoka Uingereza amepata ajali wa mbio za kufuzu za mashindano ya Grand Prix ya Ujerumani. Dereva huyo wa timu Mercedes alipoteza mwelekeo katika hatua za mwanzo na kugonga nguzo zilizoko pembezoni mwa barabara zinazotumika mashindano hayo. Hamilton alitoa taarifa kwa wenzake kupitia redio kuwa breki zake zilishindwa kufanya kazi kabla ya kuchukuliwa na kuepelekwa katika kituo cha afya kwa uchunguzi. Dereva huyo ambaye yuko nyuma ya dereva mwenzake Nico Rosberg kwa alama nne kuelekea katika mbio za ubingwa, anatarajiwa kuanza katika nafasi ya 15 katika mbio hizo zitakazohitimishwa kesho. Katika mashindano hayo ya kufuzu Rosberg ndiye aliyeibuka kidedea akifuatiwa na dereva wa timu ya Williams Valtteri Bottas wakati Felipe Massa wa timu ya Ferrari alimaliza katika nafasi ya tatu.
No comments:
Post a Comment