 |
Faulo aliyofanyiwa Neymar. |
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar atakosa mechi zilizosalia za nchi hiyo katika michuano ya Kombe la Dunia kutokana na kupata majeruhi ya mgongo. Mfupa wa nyota huyo unaoshikana na uti wa mgongo ulivunja mwishoni mwa mchezo war obo fainali dhidi ya Colombia ambao walishinda mabao 2-1 na kutolewa nje kwa machela ambapo alipelekwa moja kwa moja hospitali.
 |
Mfupa wa uti wa mgongo uliovunjika. |
Kumkosa Neymar itakuwa pigo kubwa kwa Brazil katika mchezo wao nusu fainali dhidi ya Ujerumani kutokana na pia kumkosa nahodha wake Thiago Silva ambaye ana kadi mbili za njano. Ujerumani wao walitinga hatua hiyo baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa katika mchezo mwingine war obo fainali uliochezwa mapema.
No comments:
Post a Comment